
Kuishi na VVU
Ukiwa na matokeo yanayosema una VVU unaweza kuwa na hasira, kuchanganyikiwa au hofu. Lakini kwa taarifa sahihi, msaada na matibabu, unaweza kuishi maisha marefu na yenye afya.
Matibabu ya VVU yakitumiwa kila siku husaidia mfumo wa kinga na kupunguza virusi mwilini.